MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amekabidhiwa jumla ya ngombe 500 na mbuzi 1000 na Jumuiya ya IDDEF ya nchini Uturuki kwa ajili ya sadaka ya kusherekea sikukuu ya Eid al-Adha.
“Jumuiya ya IDDEF tumetoa ngombe 500 na mbuzi 1000 kama Sadaka ya kusherekea idi alhaji kwa ajili ya kuchinjwa na kugawanywa kwa watu wa makundi mbalimbali ikiwemo wahitaji siku y kusherekea Idi” alisema
Aidha aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kukubali msaada huo na kutoa machio hiyo kwa ajili ya kuchia wanyama hao.
Akipokea msaada huo, Kunenge aliishukuru taasisi hizo kwa sadaka hiyo ya ibada ya kuchinjwa ya Idi Alhaj na kwamba sadaka hiyo itagawanywa kwa wahitaji ikiwemo, yatima,wajanena na wazee.
“Nimepokea Ngombe 500 na mbuzi 1000 Kwa ajili ya sadaka ya ibada ya kuchinjwa ya Idi Alhaji naipongeza Jumuiya hii na mashehe wote kutoka Uturuki kuendelea kushirikiana na nchi yetu katika nyanja mbalimbali”alisema.
Mbali na hilo kunenge alisema ni vema sadaka hizo zikatolewa kwa wahitaji ikiwemo yatima,wajane, wazee, watu wasiojiweza ikiwemo waalimu wa dini.
Kwa upande wake mwakilishi wa Shekhe wa Mkoa wa Pwani, Salimini Buda, aliishukuru taasisi hiyo na kwamba Sadaka hiyo itawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa.