IEA : Tudhibiti mgogoro wa nishati

MKUU wa Shirika la Nishati la Kimataifa (IEA), Fatih Birol ametahadharisha kuwa mgogoro unaoendelea wa nishati Mashariki ya Kati unaweza kushusha uchumi wa dunia ikiwa hali hiyo haitatatuliwa haraka.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Canberra, Australia, Birol aliulinganisha mgogoro wa sasa na ule wa nishati wa miaka ya 1970 na athari za uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine mwaka 2022.SOMA: Rais Samia ashiriki mkutano wa Italia, Afrika
Birol amesema kwamba karibu vituo 40 vya nishati vimeharibiwa kwa kiasi kikubwa Mashariki ya Kati kutokana na vita vinavyoendelea. “Tunakabiliwa na migogoro miwili ya mafuta na mmoja wa gesi yote yakiwa yameunganishwa, hali ni tete ” amesema Birol.
Mkuu huyo wa IEA ameongeza kuwa shirika lake linafanya mazungumzo na serikali za Asia na Ulaya kuhusu kutolewa kwa mafuta kutoka kwenye akiba ya kimkakati iwapo itahitajika.Mataifa wanachama wa IEA walikubaliana Machi 11 kutoa mapipa milioni 400 ya mafuta kutoka kwenye hifadhi za kimkakati ili kupunguza kupanda kwa bei za mafuta ghafi duniani.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com