IGP afanya mabadiliko ya Makamanda

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura amefanya mabadiliko madogo ya kuwahamisha baadhi ya Makamanda wa Polisi.
Akitoa taarifa hiyo, msemaji wa wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime leo, amesema, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Ulrich Matei ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, amehamshiwa makao makuu ya Polisi Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Benjamini Kuzaga.
Pia IGP Wambura amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), George Katabazi kutoka Makao makuu ya Upelelezi Dodoma kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara. ACP Katabazi anachukua nafasi ya ACP Benjamini Kuzaga, aliyehamishiwa Mbeya.
Amesema mabadiliko hayo yalianza Septemba 8, 2022 na ni katika kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya Jeshi la Polisi.