IHI yazindua rejesta kwa watoto wachanga

IFARAKA Health Institute (IHI) imezindua rejesta itakayotumika kukusanya taarifa za watoto wachanga.

Akizungumza Dar es Salaam Leo kwenye uzinduzi huo, Mkurugenzi wa IHI, Dk Honorati Masanja amesema rejesta hiyo itawasaidia kupata taarifa zinazohusiana na matatizo mbalimbali na vifo vya Watoto wachanga.

“Mpango huu umeanza hapa Dar es Salaam na tutasambaza katika hospital izote ambazo zinatoa huduma ya Watoto wachanga. Mpango uliopo baada ya kuzifanyia kazi zitasambazwa kwingine kwasababu vitabu vinahitaji kuchapishwa, hilo ni jukumu la serikali, wizara ya afya na Tamisemi,”amesema Dk Masanja ambaye pia, ni mratibu wa kitaifa wa mpango wa Nest360 Tanzania.

Takwimu za sasa zinaonesha kuwa katika kila vizazi hai 1000 watoto 24 wanapotea hivyo, malengo endelevu yanawadai mwaka 2030 wawe wamefika nusu ya hivyo vifo yaani 12 au kushuka chini kwa hiyo amesena wanahitaji kuongeza nguvu na kasi.

Kwa upande wake, Mratibu wa huduma za afya ya mtoto mchanga wa Wizara ya Afya Dk Angela Leonard amesema pendekezo la kuandaa rejesta hiyo lilitoka mwaka 2018 na hii ni kutokana na data walizokuwa nazo kuonesha idadi watoto wachanga wanaofariki ni wengi.

Amesema serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (Tamisemi) inaendelea kutoa mafunzo kwa watoa huduma namna ya ujazaji wa rejesta. Tayari hatua ya kwanza wamefundisha kwa njia ya mtandao kwa waratibu wa mikoa yote.

Amesema wanaendelea kuchapisha vitabu na wako katika hatua za kusambaza.

Mwakilishi wa Tamisemi Mary Shadrack ameshukuru wadau wote walioshiriki pamoja kuandaa hizo rejesta itawasaidia kama watekelezaji na watungaji wa sera kuanza kuwajua na kuwatambua watoto waliozaliwa na ulemavu wa aina yoyote.

“Tunaona mambo makubwa ambayo hatukuwa nayo hapo awali, tulikuwa kwenye rejesta ya zamani ambazo hujui watoto waliozaliwa au kufa ni kwasababu zipi lakini hii ya sasa itatupa nafasi ya kujua alipata changamoto gani,”amesema.

Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) Professa Emevitus Manji amesema amesema kwa muda mrefuTanzania kulikuwa na ufinyu wa kupata taarifa za watoto wachanga, sasa mambo yatakuwa mazuri itasaidia serikali kupanga mikakati yake vizuri.

“Takwimu zilikuwa zinaandikwa kwenye vikaratasi kama vya kuandika karanga au kwenye vibox kwa hiyo nyingine zilikuwa zinapotea hatujui wangapi wanazaliwa wangapi wamepata matatizo, serikali ilikuwa inapata tabu kuweka mikakati,”amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button