MKUU wa Jeshi la Polisi (IJP), Camillus Wambura amewahamisha makamanda wa polisi mikoa miwili na mmoja kamhamishia makao makuu ya Polisi Dodoma.
Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime jana ilieleza kuwa amemhamisha Henry Mwaibambe ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita kwenda Mkoa wa Tanga kuwa Kamanda wa Polisi mkoa huo.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Shomary amehamishiwa Mkoa wa Geita kuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa huo.
Aidha, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Richard Ngole amehamishiwa makao makuu ya Polisi Dodoma. Nafasi yake imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Kungu Malulu aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji.