MAREKANI : SHIRIKA la Kimataifa la Fedha, IMF, limetoa ombi maalum kwa serikali ya Kenya kuchunguza madai ya ufisadi na utawala bora ili kujiridhisha kutoa mikopo mingine iliyokwama.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hilo kwa vyombo vya habari imesema mkopo wa takriban dola milioni 600, chini ya IMF, na ambao muda wake unamalizika mwaka 2025, umekwama tangu serikali ilipositisha mpango wake wa kukusanya dola bilioni 2.7 kupitia makusanyo ya kodi kufuatia maandamano ya kitaifa.
SOMA : Wasiwasi ma Gen Z wakijiandaa kuandamana tena
Zaidi ya watu 50 walifariki dunia katika maandamano hayo yaliyoishindikiza serikali kuhusu mswada wa fedha uliofichua matumizi mabaya ya fedha za umma na uwajibikaji mdogo wa viongozi.
Wizara ya fedha nchini Kenya haijasema lolote hadi sasa kuhusu ombi hilo.