INDIA : Mkanyagano wa Ibada wauwa watu 15

INDIA : ZADI ya watu 15 wamefariki kwenye mkanyagano katika mkusanyiko mkubwa wa kidini  huku wengine wakijeruhiwa.

Mahujaji wa kihindu walikuwa wakikimbilia mito mitakatifu kwa ajili ya ibada ya kujitakasa, waliwakanyaga watu waliokuwa wamekaa pembezoni mwa mito hiyo na kusababisha janga hilo.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa wazee na wanawake ndio wengi walikanyagwa na hakukuwa na msaada wowote.

Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kutuma salamu za rambirambi kwa familia  zilizopoteza ndugu zao.

SOMA: India yazungumzia amani, usalama BRICS

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button