INEC yafungua milango fomu za udiwani Geita

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Agosti 19, 2025 imeanza kutoa fomu kwa wagombea wa nafasi ya udiwani wilayani Geita waliopitishwa na vyama vyao kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu 2025.

Idadi kubwa ya wagombea waliojitokeza kuchukua fomu siku ya jana ni kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao kila mmoja ametumia nafasi yake kushukuru kwa kuaminiwa kupeperusha bendera ya CCM.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu jana, Mgombea Udiwani Kata ya Butobela Paschal Mapungo amesema imani aliyopewa na chama na wananchi ni kubwa na inatoa deni kwake kupigania ushindi.

Mapungo amesema deni hilo halikomei kwenye kusaka ushindi katika uchaguzi mkuu pekee bali pia inampa nguvu ya kuwapigania wananchi kusukuma gurudumu la maendeleo kwa kujenga ushirikiano wenye tija.

Aidha amewaomba wajumbe, viongozi na wanachama wengine waliokuwa wametia nia ndani ya chama kuachana na makundi na kuunganisha nguvu kufanikisha ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu.

“Mimi nawaambia watia nia ambao tulikuwa nao kwenye kinyanganyiro ndani ya CCM, tushirikiane kwa pamoja, tofauti zilizokuwepo tuziweke kando tuwe kitu kimoja.

“Sisi ni kitu kimoja dhamira yetu kuu ni kuchukua dora katika kata ya Butobela, na niaimani kwa kata hii jambo hilo hatuna, tulishatoa tofauti zetu, CCM ni wamoja, tupo tayari kupigania chama chetu”, amesema.

Kwa upande wake Mgombea Udiwani kata ya Bombambili, Leornard Bugomola amesema ni nafasi nyingine aliyopewa na CCM ni kithibitisho kikubwa cha imani ya utendaji na uwajibikaji bora

Naye Mgombea Udiwani kata ya Kalangalala, Ruben Sagayika amesema akiwa kama kijana anaamini anao wajibu wa kuwasaidia vijana kupitia nafasi ya udiwani na ndio maana amewiwa kuchukua fomu.

Aidha Mgombea Udiwani kata ya Ludete, Jumanne Misungwi amesema ikiwa hii ni mara ya kwanza anaingia kwenye kinyanganyiro cha udiwani anatamani kutoa msaada kwa wananchi kupitia utumishi bora.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button