Infantino yupo Fifa hadi mwaka 2027

RAIS wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) Gianni Infantino amechaguliwa tena kuongoza shirikisho hilo hadi mwaka 2027 katika kongamano la FIFA nchini Rwanda.

Licha ya kuungwa mkono na wanachama nchi kadhaa za Ulaya zikiwemo Ujerumani na Uswisi hazifurahishwi na wadhifa wake, zikidai hazitamuunga mkono kikamilifu.

Nawapenda nyote,” Infantino aliwaambia wajumbe katika mji mkuu wa Rwanda, ambapo mfumo wa upigaji kura haukusajili idadi ya wapinzani.

Advertisement

Wakati sheria za FIFA kwa sasa zinaweka kikomo cha rais hadi mihula mitatu, minne, Infantino tayari ameandaa mazingira ya kusalia hadi 2031, akitangaza mnamo Desemba kwamba miaka yake mitatu ya kwanza kwenye madarakani haikuhesabiwa kama muhula kamili.

Michuano ya Kombe la Dunia kwa wanaume itaongezeka kutoka timu 32 hadi 48 mwaka 2026, wakati Kombe la Dunia la Wanawake litashirikisha timu 32 kwa mara ya kwanza huko Australia na New Zealand mwaka huu

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *