Iran, E3 waanza mazungumzo mapya

TEHRAN : WANADIPLOMASIA wa Iran wanakutana leo na wenzao kutoka Ujerumani, Uingereza na Ufaransa kwa mazungumzo mapya kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, hatua inayokuja baada ya mataifa hayo ya Magharibi (E3) kuionya Tehran kwamba yanaweza kurejesha vikwazo vilivyofutwa mwaka 2015 iwapo haitakubali masharti ya mazungumzo mapya.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baqaei, amesema mkutano huo unaofanyika Istanbul ni fursa ya Ulaya “kujipima upya na kurekebisha mtazamo wake kuhusu masuala ya nyuklia ya Iran.” SOMA: Mpango wa Nyuklia Iran watingisha Marekani

Huu ni mkutano wa kwanza tangu Israel ilipoishambulia Iran Juni 13, ikilenga vinu vya nyuklia na makambi ya kijeshi, shambulizi lililosababisha vita vya siku 12 na kuchelewesha mazungumzo ya awali kati ya Tehran na Washington yaliyokuwa yameanza Aprili.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button