Mpango wa Nyuklia Iran watingisha Marekani

MAREKANI : RIPOTI ya ujasusi ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani imeeleza kuwa mashambulizi ya anga dhidi ya vinu vya nyuklia vya Iran hayakuweza kuuharibu mpango huo, bali yaliuchelewesha kwa muda mfupi wa mwezi mmoja hadi miwili.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kiusalama vilivyozungumza na shirika la Reuters, hifadhi ya urani ya Iran haikuathirika, hivyo taifa hilo bado lina uwezo wa kuendeleza mpango wake wa nyuklia licha ya mashambulizi hayo.
Hali hii inajiri wakati makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Iran yakiwa yanasuasua, huku kila upande ukijitangaza mshindi. Waangalizi wa kimataifa wanasubiri kuona iwapo mzozo wa Mashariki ya Kati utatulia au kuendelea.