Iran, Marekani kurejea kwenye mazungumzo

ROME : IRAN imetangaza kuwa inatarajia kurejea mezani na Marekani kwa mazungumzo kuhusu mpango wake wa nyuklia, yatakayofanyika mjini Rome, Italia, mwishoni mwa wiki hii.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema leo kuwa duru mpya ya majadiliano hayo, ambayo yanasimamiwa na nchi ya Oman, imepangwa kufanyika Jumamosi katika mji huo mkuu wa Italia.
Hata hivyo, hadi sasa Serikali ya Marekani haijatoa taarifa rasmi kuthibitisha ushiriki wake katika mazungumzo hayo yaliyosimamishwa kwa muda mrefu.
Aidha, mkutano mwingine unatarajiwa kufanyika Ijumaa, siku moja kabla ya majadiliano kati ya Iran na Marekani, ambapo wawakilishi wa mataifa ya Ujerumani, Ufaransa na Uingereza watakutana kujadili suala hilo.
Mataifa hayo ya Ulaya ni miongoni mwa yale yaliyotia saini makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015, yaliyolenga kuizuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia, na yameendelea kushinikiza kurejea kwa mazungumzo ya kidiplomasia ili kufufua makubaliano hayo.
SOMA: China, Urusi waongoza mitambo ya nyuklia