Tupo tayari kufanya mazungumzo- Iran

IRAN : WAZIRI wa mambo ya nje wa Iran, Abbas Araghchi amesema nchi yake inaweza kuwa tayari kuzungumza na utawala wa Trump licha ya utawala huo kuonyesha msimamo mkali kuelekea Tehran.
Akizungumza pembezoni mwa mkutano wa baraza la mawaziri nchini Iran, Araghchi amesema ikiwa wasiwasi mkubwa uliopo ni kuhusu kuhakikisha Iran haitengenezi silaha za Nyuklia, basi hilo ni suala linaloweza kutatuliwa.
Trump alitoa agizo la kuweka shinikizo kubwa zaidi dhidi ya Iran, linalojumuisha hatua za kuchukuliwa ikiwemo vikwazo vipya na kuviimarisha vikwazo vilivyopo.
SOMA: Iran kusaini mkataba wa kimkakati na Urusi



