LEBANON : JESHI la Israel limemuua kiongozi mwingine wa kikosi maalum cha kundi la Hezbollah,Mustafa Ahmad Shahadi katika shambulizi lililofanywa eneo la Nabatieh kusini mwa Lebanon.
Taarifa ya jeshi la Israel imesema katika shambulizi lililofanywa na jeshi la anga la Israel limemshambulia kiongozi huyo na kumuua.
Awali, kiongozi huyo alikuwa akiendesha operesheni za kikosi cha Radwan nchini Syria na kusimamia mashambulizi ya kigaidi kusini mwa Lebanon.
Wakati haya yakitokea,kiongozi mpya wa kundi la Hezbollah, Naim Qassem, amesema ataendeleza mkakati wa kivita uliowekwa na mtangulizi wake Hassan Nasrallah aliyeuwawa na vikosi vya Israel mwezi uliopita.