LEBANON : HEZBOLLAH imetangaza kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Kundi hilo, Naim Qassem atakuwa kiongozi wa Hezbollah.
Naim Qassem anachukua nafasi ya Hassan Nasrallah, ambaye aliuawa katika shambulio la anga la Israel huko Beirut mwezi uliopita.
Qassem ni miongoni mwa viongozi wachache waandamizi wa Hezbollah ambao wamesalia hai, baada ya Israel kuua viongozi wengi wa kundi hilo katika mfululizo wa mashambulizi.
SOMA : Hakuna mawasiliano na mrithi wa Nasrallah
Uteuzi huo unafanyika huku mzozo nchini Lebanon ukiendelea kuongezeka kati ya Israel na Hezbollah.