VYANZO vya habari vya usalama vya Lebanon vimesema havina mawasiliano na aliyeteuliwa kumrithi aliyekuwa kiongozi wa kundi la Hezbollah, Sayyed Hassan Nasrallah baada ya mashambulizi ya Israel yaliyoripotiwa kumlenga mrithi huyo.
Shirika la Habari Uingereza-Reuters limesema Israel imefanya shambulio kubwa katika vitongoji Kusini mwa Beirut Oktoba 3 ambalo maafisa wa Israel wamesema lilimlenga mtarajiwa huyo wa urithi, Hashem Safieddine kwenye handaki chini ya ardhi.
SOMA: Jeshi la Israel: Hassan Nasrallah amekufa
Vyanzo hivyo vya usalama vya Lebanon vimesema mashambulizi yanayoendelea ya Israel kwenye kitongoji cha Dahiyeh Kusini mwa Beirut tangu Oktoba 4 yamezuia waokoaji kufika eneo la shambulizi.
Hadi sasa Hezbollah haijatoa kauli kuhusu Safieddine tangu shambulizi hilo.