Israel yawaachilia wafungwa 183 wa Kipalestina

ISRAEL : SERIKALI ya Israel imewaachilia huru wafungwa 183 wa Kipalestina, muda mfupi baada ya Wanamgambo wa Hamas kuwaachilia huru mateka watatu wa Israel mapema leo Jumamosi.

Hatua hii ya kubadilishana wafungwa na mateka ni sehemu ya makubaliano ya pande hizo mbili ya kusitisha vita katika Ukanda wa Gaza. SOMA: Wapalestina wagoma kuhamishwa GAZA

Katika awamu ya kwanza ya usitishaji wa mapigano, iliyodumu kwa wiki sita, jumla ya mateka 33 na karibu wafungwa 2000 wanatarajiwa kuachiliwa huru. Aidha, misaada ya kibinadamu itaruhusiwa kuingia katika Ukanda wa Gaza, ambao umeathiriwa vibaya na vita.

Advertisement

Katika hatua nyingine, Wizara ya Afya ya Gaza, inayodhibitiwa na Hamas, imesema Wapalestina 50 wanaohitaji matibabu wamepelekwa Misri kupitia kivuko cha Rafah mapema leo Jumamosi. Kivuko cha Rafah, ambacho ni njia kuu ya kuingia Gaza na kupitisha misaada, kilifungwa tangu Israel ilipoudhibiti upande wa Palestina wa kivuko hicho.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *