‘Jadilianeni kwa hoja kukuza demokrasia’

VYAMA vya siasa nchini vimetakiwa kuendelea kujadiliana na kusikilizana kwa hoja mbalimbali zitakazojenga vyama vyao, pamoja na kupeana fursa  ya kutoa maoni yatakayoboresha uendeshaji wa vyama na kukuza demokrasia nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohhamed Ali Ahmed, wakati akifunga mkutano wa kikao kazi wa viongozi wa vyama vya siasa nchini ulioanza Julai 17, 2023 na kumalizika leo Julai 18, 2023 uliolenga kutoa maoni juu ya uchaguzi na maandalizi ya kuelekea kwenye uhakiki wa vyama vya siasa.

Akizungumzia lengo la mkutano huo Ahmed amesema ni kuendeleza safari ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan ya kuwapa fursa Watanzania ya kuzungumza na kutoa maoni waliyonayo, ili kujenga Tanzania yenye heshima na yenye watu wa kuheshimiana.

Amevitaka vyama vya siasa visisite kutoa maoni waliyonayo,  huku akiahidi kuendelea kuyafanyia kazi maoni yote yaliyotolewa katika kikao kazi hicho.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema bado ana wasiwasi mkubwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongozi mwaka 2024 kwasababu taratibu za kuufanya uchaguzi huo uwe wa haki na huru bado haujaandaliwa, hivyo kuiomba serikali kuandaa utaratibu huo.

Makamu Mwenyekiti  wa Chama Cha ACT Wazalendo Tanzania  Bara, Dorothy Semu amesema mkutano huo umewapa fursa nzuri ya kujua  namna bora ya kuboresha chama pamoja na kutatua changamoto za chama katika utekelezaji wa majukumu yao.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Deborahnderson
Deborahnderson
2 months ago

Single Mom With 4 Kids Lost Her Job But Was Able To Stay On Top By Banking Continuously DOLLER 1500 Per Week With An Online Work She Found Over The Internet… 

Check The Details HERE…..  https://cashonline76.blogspot.com/

Last edited 2 months ago by Deborahnderson
Julia
Julia
2 months ago

Earn money by working online. You are free to work from home whenever you choose. Working only five hours every day online, you might earn more than $600. I made $18,000 doing this in my spare time.
.
.
Detail Here===================================>>>  http://Www.OnlineCash1.Com

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x