Jafo asisitiza weledi kwenye utekelezaji wa miradi

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,
Selemani Jafo amewataka washauri elekezi wa mazingira kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na ili kufikia malengo ya utekelezaji wa miradi.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Tano wa mwaka wa Chama cha Washauri Elekezi wa Mazingira Tanzania (TEEA) uliyofanyika mkoani Dar es Salaam.
Amesema wataalamu wa mazingira ni wadau muhimu katika ajenda
ya uwekezaji ambao unategemea Cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira
(TAM) hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa ufanisi.
Aidha amesema uwekezaji wowote unahitaji andiko la cheti ambacho ni mwongozo
wa uwekezaji hivyo lazima uzingatie takwimu hasa katika masuala ya hali ya
hewa ili kutoa cheti kinachozingatia matakwa ya hali ya hewa kwa mfano
ujenzi wa madaraja unaozingatia ustahimilivu wa mvua.
 
“Naombeni niwaambie ndugu zangu, leo hii inawezekana kuna baadhi ya watu
hawajui thamani yenu ninyi wataalamu wa mazingira tunashuhudia katika
kipindi cha miaka mitatu, miradi 7,195 imetekelezwa kwa sababu mmeifanyia
tathmini,” amesema waziri Jafo

Ameongeza kuwa miradi yote yenye kuhitaji uwekezaji wa mashirika makubwa
ya fedha duniani hauwezi kupata fedha bila kuwa imefanyiwa ukaguzi na
kupata vyeti vya TAM.

Pia waziri Jafo amewataka wataalamu hao kutoa ushauri wa mazingira kwa
wawekezaji ili kuwepo na uwekezaji wenye tija na manufaa katika jamii huku
akisema mfumo wa kusajili miradi umekuwa na mafanikio.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TEEA, Emmanuel Hanai amesema
wataalamu elekezi hao wakitumiwa vizuri watakuwa mfano mzuri katika
kuelimisha jamii kulinda mazingira.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button