Jahazi la JKT lazidi kuzama kikapu Afrika

MWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kufuzu klabu bingwa Ligi ya Kikapu Afrika (BAL) timu ya JKT imepoteza mchezo wa pili dhidi ya GNBC ya Madagascar kwa pointi 89-72.

Mchezo huo uliofanyika kwenye viwanja vya Filbert Bayi vilivyopo eneo la Mkuza, Kibaha mkoani Pwani, ulikuwa wenye ushindani mkali baina ya timu zote mbili ambapo Meneja wa JKT Seif Ngowi amesema timu yake ingeshinda lakini wachezaji walikosa umakini.

“Tuliongoza robo ya kwanza, ya pili wakachukua wapinzani lakini ya tatu na nne tulikimbizana na kutofautiana pointi moja mpaka mbili. Kupoteza kwetu kumetokana na makosa ya wachezaji hawakutaka kufuata maelekezo,”amesema.

SOMA: JKT yaanza vibaya michuano ya Afrika

Licha ya kupoteza, amesema bado hawajakata tamaa kuna michezo miwili imebaki dhidi ya Nairobi City Thunders ya Kenya na Beau Vallo Heat ya Ushelisheli wanayotakiwa washinde ili wapate nafasi angalau ya mshindwa bora (best looser) kuvuka hatua ya nane bora.

Timu inayoongoza kundi ni Urunani BBC ya Burundi iliyoshinda michezo miwili huku Nairobi City na GNBC kila mmoja zikishinda mchezo mmoja.

Urunani katika mchezo wa pili imeshinda kwa pointi 112-43 dhidi ya Beau Vallon heat.

Michezo ya leo jioni ni Beau dhidi ya GNBC na Urunani dhidi ya Nairobi City.

Habari Zifananazo

Back to top button