Jaji Afrika Kusini afunguliwa mashtaka

BUNGE la Afrika Kusini limemfungulia mashtaka mmoja wa majaji wakuu wa nchi hiyo kwa utovu wa nidhamu.

Uchunguzi uligundua kuwa John Hlophe, jaji mkuu katika jimbo la Western Cape, alijaribu kushawishi majaji katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo katika kesi inayomhusu Rais wa zamani Jacob Zuma.

Aliwasiliana na majaji wawili mwaka 2008 ili kuona kama wangemuunga mkono Zuma katika uamuzi unaohusiana na kesi ya ufisadi.

Hlophe mar azote amekuwa akikikanusha shtaka hilo.

Kucheleweshwa kwa muda mrefu kati ya kosa linalodaiwa na kushtakiwa kwake kulitokana na rufaa ya muda mrefu na uchunguzi.

Rais Cyril Ramaphosa sasa atalazimika kusaini uamuzi huo na kupanga tarehe ya kuondolewa kwake rasmi.

Habari Zifananazo

Back to top button