Jaji aizuia serikali kufunga USAID

MAREKANI: JAJI mmoja wa Marekani ameizuia serikali ya Marekani na bilionea Elon Musk kutochukua hatua zaidi za kulifunga Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani (USAID), akisema kuwa hatua hiyo inaweza kuwa inakiuka katiba ya nchi.

Katika uamuzi wa awali uliofanywa na Jaji Theodore Chuang katika jimbo la Maryland, aliamuru kuwa wafanyakazi wa kudumu wa shirika hilo pamoja na wale wanaofanya kazi kwa mikataba, wakiwemo maelfu waliosimamishwa kazi, warudishiwe haki zao za mifumo ya kompyuta.

Uamuzi huu wa jaji unakuja kufuatia kesi zilizowasilishwa mahakamani na wafanyakazi wa sasa na wa zamani wa USAID, ambao walikataa hatua ya kufutwa kazi na kusimamishwa kwao, hatua ambazo waliziita kuwa za kikatili na zisizo za kisheria.

USAID, shirika linalohusika na utoaji wa misaada ya kibinadamu na maendeleo katika maeneo mbalimbali duniani, limekuwa likikumbwa na changamoto kubwa tangu bilionea Elon Musk kuhusishwa na juhudi za kifedha na kisiasa za kubadilisha muundo wake.

SOMA: Mwinyi aiomba UNESCO kusaidia uchumi wa Buluu Zanzibar

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button