Jamii yahakikishiwa usalama chanjo ya polio

GEITA: SERIKALI imeihakikishia jamii mkoani Geita kuwa chanjo ya kinga dhidi ya ugonjwa wa polio ni salama na imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Wizara ya Afya Nchini.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mkuu wa wilaya ya Geita Hashimu Komba ametoa taarifa hiyo katika uzinduzi rasmi wa chanjo ya polio katika shule ya Msingi Juhudi katika Manispaa ya Geita.

Amesema mara zote kunapokuwa na kampeni ya utoaji wa chanjo zimekuwa zikiibuka taarifa za upotoshaji zenye nia ya kukwamisha zoezi lakini jamii inapaswa kuzipuuza ili kufanikisha zoezi.

Amesema kampeni ya chanjo ya polio kwa watoto chini ya miaka 10 ni sehemu ya juhudi za serikali kuikinga jamii dhidi ya magonjwa ya mlipuko ili kufikia azma ya kuimarisha afya ya jamii.

“Tumekuwa na chanjo mbalimbali kwenye taifa hili, na chanjo zote zinazokuja kwenye taifa letu ni chanjo salama, ni chanjo ambazo hazina madhara, zinalenga kuimarisha king ana afya za watu”, amesema.

Komba amewaomba viongozi wa dini zote kutumia nafasi yao kuhamasiha na kuelimisha waumini kwenye nyumba za ibada kuhusu dhamira njema ya serikali kutoa chanjo ya polio kwa watoto.

Aidha amewataka viongozi wote wa kijamii na vyama vya siasa kushiriki kufanikisha chanjo hiyo ambayo imekuja baada ya kugundulika kirusi cha polio kwenye maji taka mkoani Mwanza.

Amesema Geita imelenga kutoa chanjo ya polio kwa watoto 1,114,918 na ambapo imepokea jumla ya zaidi ya dozi za chanjo milioni 1.3 ambazo zinatosheleza mahitaji yote kusudiwa.

Mganga Mkuu wa mkoa wa Geita, Dk Omari Sukari amesema watoa huduma za afya zaidi ya 6,000 wameandaliwa na utekelezaji unaanza mara moja Machi 24, 2026 kwa kufuata miongozo ya afya.

Ofisa Mpango wa Taifa wa Chanjo Wizara ya Afya, Anna Kajiru amesema maandalizi ya utoaji chanjo yamekamilika kuhakikisha zoezi linazifikia kaya na shule zote kwenye mikoa saba inayolengwa.

Anna amekiri kuwa mpaka sasa mkoa wa Geita imekuwa kinara wa maandalizi ya chanjo ya polio na mwitikio wa ushiriki wa viongozi wa kijamii umetoa tumaini la kufanikisha chanjo hiyo.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button