Jamii yashauriwa kutumia urejeshwaji taka kuanzisha miradi

JAMII imeshauriwa kutumia fursa ya urejeshwaji wa taka katika kuanzisha miradi mbalimbali itakayowasaidia kuondokana na changamoto za kiuchumi kwani taka hizo ni malighafi inayoweza kutumika kwa matumizi mengine.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Thomas Chali ametoa wito huo Dar es Salaam, leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika kilele cha Siku ya Mazingira duniani, kilichofanyika eneo la ambayo pia imeambatana na usafi wa mazingira katika ufukwe wa Coco.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria kutoka Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira ( NEMC )Jamali Baruti amesema kuwa kwa mujibu wa Takwimu walizonazo Tani elfu-29 zinasababisha uchafuzi wa Mazingira na kuua viumbe hai baharini kwa mwaka na kwamba chanzo kikubwa ni matumizi ya plastiki.
Nao Mwakilishi wa Shirika la Mazingira Umoja wa Mataifa Duniani Tanzania (UNEP), Clara Makenya na Mkurugenzi wa Asasi ya kiraia inayohusika na Mazingira Hudefo, Sarah Pima wamesema lengo la kuandaa maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani ni kuendelea kutoa elimu kwa vijana juu ya fursa
zinazopatikana katika urejeshwaji wa taka.
Wameshauri serikali kuzingatia suala la takwimu ili kuwepo na maamuzi sahihi juu ya kukabiliana na changamoto ya matumizi ya plastiki nchini.



