Japan kuendeleza mafunzo,miradi nchini

BALOZI wa Japan nchini Tanzania, Misawa Yasushi amesema kupitia Shirika la Maendeleo la Japan Tanzania(JICA ) wataendelea kutoa mafunzo ya ujuzi kwa Watanzania na kuwezesha miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.

Tangu kuanzishwa kwa JICA 1962 hadi mwaka 2022 jumla ya wanafunzi wa Kitanzania 147,863 wamepewa ufadhili wa masomo na shirika hilo katika nchi mbalimbali duniani.

Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wanafunzi waliopata ufadhili wa JICA ( JATA) Yasushi amesema wanaendelea kufanikisha miradi kupitia wanafunzi waliowapa ufadhili ikiwemo mradi wa Hatua project.

Advertisement

“JICA imechangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii ikijikita katika rasilimali watu na kumekuwa na fursa nyingi za mafunzo na miradi na siku ya leo ninafuraha kushiriki na kujua kutoka kwa wanachama wa JATA ambapo kuna miradi kama HATUA ulioanzishwa kutatua matatizo ya wananchi nah ii inaendana na mikakati yetu,”amesema.

Amesema tayari wadau kutoka Japan na serikali walijadili kuhusu changamoto za kiuchumi na kijamii ambapo wataweza kufanikiwa kutokana na ujuzi waliotoa na uzoefu walionao.

Kwa upande Mwenyekiti wa JATA ,Gregory Mlay amesema wamekutana kujadili mambo mbalimbali ambayo wamefanya katika miradi yao kadhaa na kazi mbalimbali kuweza kusaidiana na serikali kuleta maendeleo na kuelimisha jamii ikiwemo kilimo ambapo wana wataalamu mbalimbali .

“Tunakutana na wananchi tofautitofauti tunaangali mambo tuliyofanya mwaka uliopita na kupanga kwa mwaka unaofata na tayari tumefanya miradi na wavuvi Zanzibar JICA walijenga soko la Malindi na wavuvi wengi wanafaidika kutokana na changamoto iliyoibuliwa na JATA pia wakulima walikuwa wanafanya kilimo na wanapata hasa JICA imesaidia kuwafundisha kuanzia sokoni na kwenda kulina kuna miradi mingi zaidi.

Amewasisitiza wataalamu wengine kuwa na umoja kwani watanzani wengi wanalalamika hakuna ajira wakiwa pamoja ni rahisi kubuni miradi na kutumia elimu waliyopata katika mazingira yao wakikutana wanaungana na kupata mawazo mazuri.

Naye Mwakilishi wa JICA Tanzania,Ara Hitoshima amesema JATA ni viungo muhimu katika kufanya kazi zao hapa nchini ambapo wataendeleo kutoa mafunzo na kutktleza miradi ya maendeleo.

“JATA ni kama daraja la kwenda kwa wananchi tunafanya kazi kwa pamoja kufanikisha miradi kwani wao waanenda ndani ya jamii na kuangalia changamoto na kubuni suluhu ambazo tunashiriki pamoja. Amewasisitiza wananchama wa JATA kuendelea kubadilishana ujuzi na uzoefu ili lengo la kupata mafunzo lifanikiwe.