Jela miaka 30 kwa kumnajisi mtoto

MKAZI wa kijiji cha Kijiweni, wilayani Sengerema, mkoani Mwanza, Masele Maganga ,42, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumnajisi mtoto wa miaka sita (jina limehifadhiwa).

Hukumu hiyo imesomwa jana Februari 26,2024 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Sengerema, Evod Kisoka mbele ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Nyamhanga Tissoro Katika kesi hiyo ya jinai namba 22850/2024.

Awali, Mwendesha Mashtaka aliieleza mahakama kwamba mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 25, 2024, katika kijiji cha Kijiweni, wilayani Sengerema mkoani Mwanza na alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Julai 12, 2024 na kusomewa shtaka hilo ambapo alikana kutenda kaso hilo.

Baada ya Mahakama kupitia vifungu vya sheria sambamba na ushahidi uliowasilishwa na upande wa Jamhuri ikiwemo ripoti ya Mganga aliyemfanyia uchunguzi mtoto huyo, pamoja na cheti cha kuzaliwa cha mhanga, Mahakama imejiridhisha kuwa upande wa Jamhuri wameweza kuthibitisha shitaka bila ya kuacha shaka kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

Baada ya kutiwa hatiani mshtakiwa aliiomba Mahakama imuachilie huru kwa kuwa ni mkosaji wa mara ya kwanza na kudai kuwa alipitiwa na shetani.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu, Kisoka alimhukumu mshtakiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama ya Masele.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button