Jen,David Musuguri afariki dunia

MWANZA : MKUU wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Musuguri, amefariki Dunia leo jijini Mwanza alipokuwa akipatiwa matibabu.

Jenerali Musuguri alizaliwa  Januari 4, 1920 huko Butiama Mkoani Mara, na kutumikia nchi katika Jeshi kuanzia Mwaka 1942 hadi 1988 ambapo alihitimisha uongozi wake kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kati ya 1980 na 1988.

Alianza kazi yake kijeshi katika King’s African Rifles (KR) na Tanganyika Rifles kabla ya kujiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Advertisement

Jenerali Musuguri aliongoza majeshi ya Tanzania katika vita dhidi ya Idi Amin Dada wa Uganda Mwaka 1978, baada ya uvamizi wa eneo la Kyaka, Mkoani Kagera.

Mapambano na vita alivyoshiriki ni pamoja na Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Battle of Madagascar, Vita vya Kagera, na Battle of Simba Hills.

SOMA : Majenerali 6 waagwa rasmi JWTZ