Jen.Burhan atangaza Khartoum kuwa huru

SUDAN : KIONGOZI wa kijeshi wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, amewasili mjini Khartoum na kutembelea Ikulu ya Rais, ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu vita kuanza takriban miaka miwili iliyopita.

Burhan aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum, saa chache baada ya jeshi kurejesha udhibiti wa mji huo kutoka kwa Vikosi vya kijeshi vya RSF. “Khartoum sasa ni huru,” alisema Jenerali Abdel Fattah.

Serikali ya kijeshi ya Sudan ilikuwa imehamia Port Sudan baada ya RSF kuteka Khartoum mapema katika vita hivyo. Jeshi la Sudan limeendelea na mashambulizi makali dhidi ya RSF, likidai kurejesha udhibiti wa taasisi muhimu za serikali.

Kamanda mmoja wa jeshi aliliambia shirika la habari la BBC kwamba walilinda uwanja wa ndege na wanatarajia kuwaondoa wapiganaji waliobaki wa RSF ifikapo mwisho wa siku. Mapigano kati ya jeshi la Sudan na RSF yalianza Aprili 2023, huku RSF ikidhibiti sehemu kubwa ya Khartoum.

Mgogoro huu umeleta madhara makubwa, ambapo mamia kwa maelfu ya watu wamepoteza maisha na mamilioni wamelazimika kuyakimbia makazi yao.

Sudan imeendelea kukumbwa na machafuko ya kisiasa tangu kuondolewa kwa Rais Omar al-Bashir mwaka 2019. Tangu wakati huo, taifa hilo limepitia mapinduzi na mapambano ya wenyewe kwa wenyewe, huku harakati za kurejesha utawala wa kiraia zikiendelea kukwama kutokana na mvutano kati ya jeshi na makundi ya waasi.

SOMA: Jeshi la Sudan larejesha udhibiti wa Ikulu

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button