NIGERIA : MKUU wa Jeshi la Nigeria Jenerali Taoreed Lagbaja amefariki dunia baada ya kuugua akiwa na umri wa miaka 56.
Akitangaza kuhusu taarifa ya kifo cha Mkuu wa Jeshi la Nigeria, Jenerali Taoreed Lagbaja,Rais wa Nigeria Bola Tinubu amesema Jenerali Taoreed Lagbaja aliaga dunia usiku wa kuamkia leo jijini Lagos.
Jenerali Taoreed Lagbaja ameacha mke, Mariya, na watoto wao wawili.