Jengeni chama acheni kujisifu -M/kiti CCM Tanga

KOROGWE, Tanga: Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, Rajab Abdulrahaman amewataka wagombea waliopata nafasi za kuteuliwa na chama hicho kuacha kujigamba na badala yake wajikite katika kuimarisha chama.

Kauli hiyo aliitoa wakati wa mkutano wa pamoja wa kamati za kampeni ngazi za kata, wilaya na mkoa na kuongeza kuwa hakuna nafasi ya kupumzika ni kujenga chama tu.

Aliwataka wagombea hao kuhakikisha vipaumbele vyao viwe ni kuhakikisha wanamaliza changamoto za huduma za kijamii kwa wananchi lakini na kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya chama.

“Huku kwenye chama hakuna mbora au kujiona tayari kwa nafasi uliyonayo unaweza kuwavimbia watu na kujiona bora wote lengo letu ni kuhakikisha tunakijenga chama kupitia sera zake zilizopo,”alisema mwenyekiti huyo.

Hivyo aliwataka wagombea wote kuhakikisha wanafikia lengo la chama la kupata ushindi wa kura nyingi kwenye maeneo yao hususani kwa nafasi ya Mgombea wa Urais Samia Suluhu.

Twendeni tukakipiganie chama ili kiweze kupata ushindi wa kishindo badala kuanza kuvimba na kuwa mtu wa majivuno kwani chama kimekuamini kuwa utaweza kuwa suluhu ya kutatua kero za wananchi kwenye eneo lako,”amesema mwenyekiti.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button