BURKINA FASO : VIKOSI vya kijeshi nchini Burkina Faso vimeanzisha uchunguzi baada ya vidio zilizosambaa mitandaoni ambazo zinaonyesha watu waliovalia sare za jeshi wakikata mwili wa binadamu.
Tukio hilo limezua mjadala katika mitandao ya kijamii nchini humo ambapo uongozi wa jeshi umeziomba mamlaka husika kuzichunguza vidio hizo ili kuwabaini wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria.
Katika vidio hizo zilizosambaa mitandaoni hazikuonyesha tukio hilo limefanyika wapi bali walionyesha wanajeshi wamevalia sare za kijeshi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi imeeleza kuwa tukio hili ni baya na linakwenda kinyume na maadili ya kijeshi.