URUSI : JESHI la Urusi limetangaza kuviteka vijiji viwili zaidi nchini Ukraine na kudai kupiga hatua ya kusonga mbele katika eneo la mapigano la Kusini Mashariki mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa mtandao wa Telegram wa Jeshi la Urusi limeandika kuwa vikosi vyake vimetwaa udhibiti wa kijiji cha Novodarivka kilichoko Kusini mwa mkoa wa Zaporizhizhia na cha Romanivka kilichoko mkoa wa mashariki wa Donetsk.
Kadhalika Urusi imeshambulia miundo mbinu ya nishati ya Ukraine kwa droni za kijeshi usiku wa kuamkia leo katika mji wa Ternopil ambako mtu mmoja ameuwawa na wanne kujeruhiwa.
Kwa upande wake Ukraine imesema vikosi vyake vilizuia juhudi za Urusi kuvuka mto Oskil kuingia Kaskazini Mashariki mwa Ukraine. SOMA : Ujerumani yaahidi dola milioni 680 kusaidia Ukraine