Jiji la Arusha kuzisaidia klabu, vyama vya michezo

ARUSHA: MKURUGENZI wa Jiji la Arusha, John Kayombo amezitaka klabu na vyama vya michezo kuwasilisha mipango kazi yao ili viweze kusaidika kwa maendeleo ya michezo.
Akizungumza katika bonanza la michezo la Sabasaba lililofanyika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Baraa iliyopo Moshono jijini hapa, Ofisa Michezo na Utamaduni jiji la Arusha, Benson Maneno ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi wa Jiji la Arusha John Kayombo, alisema Ofisi yake imejipanga kuweza kuzisaidia timu na vyama ambavyo vitakuwa tayari kupeleka mipango kazi yao kwa ajili ya faida ya michezo jijini Arusha.
“Tumejipanga kuhakikisha Arusha inapiga hatua katika michezo ikiwemo kuwa na timu ya Ligi Kuu na kuifanya kurejesha heshima yake kama zamani ilipokuwa na timu za AFC,977KJ FC,Palsons FC, ambapo kwa kuanza wameanza na ujenzi wa uwanja wa Soka ambayo inajengwa New Arusha City,” amesema Maneno.

Alisema halmashauri ya jiji iko tayari kushirikiana na mdau yeyote ambaye yuko kuwekeza katika michezo na niwaombe Klabu na vyama kupeleka mipango kazi yao na ofisi hiyo itakuwa tayari kutoa ushirikiano.
Katika hatua nyingine Halmashauri ya Jiji la Arusha imeweka wazi kuwa itashirikiana na timu ya Mwangaza Veterans kuboresha uwanja wa Shule ya Sekondari ya Baraa ili kutoa nafasi ya vijana na wazee kushuudia burudani.
Uwanja huo utafanyiwa maboresho katika sehemu ya kuchezea (pitch) lakini pia uwekaji wa taa ambayo itatoa nafasi ya michezo kufanyika usiku ,pia itaifanya Baraa kuwa shule ya kwanza jijini Arusha kuwa na uwanja wenye taa.
“Viongozi wa Mwangaza mje jumanne tuone namna gani tunaifanyia kazi suala ili la kuboresha uwanja ili kutoa nafasi ya soka kuchezwa”.ameongeza Maneno.
Haruni Kidungu, katibu wa Mwangaza Veterans ambao ndio waandaaji wa bonanza hilo , alisema kufanyiwa maboresho uwanja wa Baraa utatoa fursa kwa wadau wa michezo Arusha kuweza kushuudia burudani ya soka kutoka kwa vijana na wachezaji wa zamani (veterans).
“Tunatarajia kuwasiliana na Ofisi ya mkurugenzi wa jiji kuboresha uwanja huu wa Baraa na bahati nzuri afisa michezo amekuwepo leo na kututaka twende jumanne naamini ombi letu litafanikiwa na tutaiboresha kwa ajili ya faiida ya visazizi vijavyo”,ameeleza Kidungu.
Naye Fredrick Lyimo “Deco” ,ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Wilaya ya Arusha Mjini (ADFA),ameipongeza Mwangaza Veterans kwa kwa kuandaa bonanza ambalo linajumuisha umoja na kusema Uongozi wake wako tayari kutoa ushirikiano muda wowote kwa timu zote Arusha.
Bonanza hilo la Sabasaba limefanika kwa mara ya sita likilenga kuwaweka pamoja wachezaji wa zamani na kudumisha umoja , lilishirikisha timu sita za Mwangaza,AICC Kijenge,KMKM ya Zanzibar,Free Stress ya Dar na Chuo Kikuu cha Nelson Mande
Mshindi wa Sabasaba bonanza mwaka huu 2025 imekuwa ni timu ya AICC Kijenge kutoka Arusha,mshindi wa pili KMKM Zanzibar na mshindi wa tatu Mwangaza Veterans Arusha



