Jiji lajipanga uzalishaji majongoo bahari, kaa

JIJI la Tanga limejipanga kuwa kinara katika uzalishaji wa majongoo bahari, unenepeshaji wa kaa pamoja na kilimo cha mwani nchini kwa kutumia fursa ya bahari iliyopo kwenye ukanda wa pwani.


Mbunge wa Tanga Mjini na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya uchumi wa buluu pamoja na ya kupendezesha jiji hilo inayofadhiliwa na Botner Foundation.


Alisema kupitia fursa ya uchumi wa buluu wananchi wataweza kujiongezea fursa ya shughuli za kiuchumi na kujiongezea kipato kupitia fursa za ufugaji na kilimo kupitia bahari.

Advertisement


“Tanga tuna eneo kubwa la bahari, tayari mafanikio tumekwishayaona hivyo tumejipanga kuongeza uzalishaji ili tuweze kuwa vinara wa kutumia fursa za uchumi wa buluu kwa maendeleo ya watu wetu sambamba na nchi kupata mapato yake,” alisema.


Alisema kutokana na miradi ya uchumi wa buluu kufanya vizuri katika jiji hilo, wamejipanga kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ikiwemo kutoa vifaa ili kuongeza uzalishaji wa mazao hayo kwa wingi.


Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Botner, Dk Hassan Mshindo alisema kuwa wamewekeza zaidi ya Sh bilioni 7.5 katika sekta ya uchumi wa bahari pamoja na kupendezesha mandhari ya Jiji la Tanga.


“Fedha hizo kwa sehemu kubwa zimepelekwa kwa vijana ili waweze kujipatia ajira na kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira iliyopo,” alisema

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *