Jina la Kijiji Mpigamiti gumzo bungeni

Baada ya kumalizika kipindi cha Maswali na Majibu bungeni leo asubuhi, ndipo Mbunge wa jimbo Sikonge George Kakunda alipoomba mwongozo, fursa ambayo Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga hakumnyima.

Huku Bunge likiwa kimya, tayari kusikia mwongozo wa Kakunda, waliishia kuangua kicheko pale mwakilishi huyo wa Sikonge akasema ikiwa Bunge linaweza kutoa maelekezo kwa Serikali kuona namna kubadili jina la kijiji cha Mpigamiti kilichopo wilayani Liwale, Lindi kwa kuwa halina tafsiri nzuri kwa baadhi ya wabunge na jamii kwa ujumla.

Baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu pamoja na matangazo, Mbungre wa Sikonge, George Kakunda ameiomba mwongozo akidai kuwa jina la kijiji cha Mpigamiti kilichopo Liwale, Lindi lina ukakasi
Akitoa hoja yake, Mbunge huyo amesema: “Mheshimiwa (Zuber) Kuchauka ameuliza maswali hapa zaidi ya mara nne…amekuwa akitaja kijiji cha Mpigamiti.

“Mwenyekiti [Najma Giga], japokuwa jina huenda limesajiliwa kihalali lakini tafsiri ya baadhi ya wabunge na hata watu huko kwenye jamii, tafsiri inakuwa sio nzuri sana, je, Bunge lako Tukufu haliwezi kutoa maelekezo kwa Serikali kubadilisha jina la hicho kijiji?”

Baada ya Kakunda kutoa hoja yake, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga alisimama na kusema majina mengine yamebeba historia ya mahali husika huku akitolea mfano Zanzibar ambako kuna majina ambayo hayaendani na lugha ya Kiswahili.

Licha ya kwamba Serikali inaweza kuliangalia hilo, Najma amesisitiza majina hayo yamekuwa yakitumika kwa kipindi kirefu.

Habari Zifananazo

Back to top button