Kamati yataka maboresho mfumo wa ajira

DODOMA: Serikali imeshauriwa kuboresha mfumo wa ajira nchini kwa kuruhusu waombaji wenye sifa na vyeti vya ngazi mbalimbali kushiriki katika usaili wa nafasi za kazi zinazotangazwa pindi zinapojitokeza, bila kuwekewa vikwazo visivyo vya lazima vinavyotokana na kiwango cha elimu pekee.

‎Ushauri huo umetolewa leo bungeni Jijini Dodoma na Kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala,Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2025/2026 pamoja na maoni ya kamati kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 yaliyowasilishwa na Mbunge wa jimbo la Itigi (CCM) Yohana Msita kwa niaba ya Mwenyekiti wa kamati hiyo Mbunge wa jimbo la Songea mjini (CCM) Damas Ndumbaro.

‎Msita amesema hatua hiyo itasaidia kuondoa malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wasomi mbalimbali wanaodai kunyimwa fursa za kuomba na kupata ajira, licha ya kuwa na sifa zinazokidhi mahitaji ya baadhi ya nafasi hizo. Kwa mujibu wa hoja hiyo, waombaji wengi wanamiliki vyeti vinavyoweza kukidhi vigezo na masharti yaliyobainishwa katika matangazo ya ajira, lakini hukumbana na vikwazo vinavyowazuia kushiriki kikamilifu.

‎‎”Wadau wanaona kuwa kuruhusu ushindani mpana kutatoa nafasi kwa waombaji kutumia uwezo na ujuzi wao kwa vitendo, badala ya kuangalia kiwango cha elimu pekee kama kigezo kikuu, hii itasaidia pia kuongeza uwiano wa ajira na kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na wasomi nchini.” amefafanua Msita.

‎Aidha, ameeleza ni umuhimu kuendelea kuboresha mifumo ya ajira ili iwe jumuishi na yenye kutoa fursa sawa kwa wananchi wote wenye sifa stahiki.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button