DAR-ES-SALAAM
VAA sare na mume wako, mpenzi au rafiki yako ili mwoekane nadhifu machoni pa watu muwapo ofisini, kanisani au kwenye mitoko hata harusini.
Unaweza ukajiuliza je umewahi kutamani kuwa na mwonekano wa kimavazi unaonekana na mwenza wako au mpenzi wako na hujui ufanye nini? SOMA: Swahil Fashion kufanya Disemba 2 mwaka huu
Jambo ambalo wamekuwa wakilipenda watu wengi lakini hujikuta kwenye wakati mgumu hasa linapokuja suala la uchaguzi wa mavazi hayo.
Ugumu huu utokea mara nyingi katika kupata nguo ambayo inawezekana kuvaliwa na mwanamke na mwanaume bila kuleta muonekana wa hajabu ila kupendeza na kuonekana nadhifu.
Zamani hili lilikuwa likiwezekana kwa urahisi kwa kutumia vitenge lakini siku hizi jambo hili limekuwa likiwezekana kutokana na kuwapo nakshi za kila aina kwenye mitindo.
Sambamba na hilo pia mnaweza kutumia rangi za aina moja wakati mnachahua mavazi ya kuvaa.
Kuvaa nguo zinazofanana na mpenzi wako au rafiki yako haijalishi ni sehemu gani muhimu mnavaa mavazi hayo.
Mnaweza kuwa na kawaida ya kuvaa mavazi hayo katika mitoko yenu ya kawaida ya kuvaa mavazi hayo katika matembezi katika fukwe na kanisani na manunuzi mbalimbali ya bidhaa za nyumbani.
Mnaweza kuvaa tisherti na jensi au mashati yanayofanana lakini pia namaweza kushona nguo ambazo zitakuwa na naski ya khanga, kitenge aukitambaa wote mkaonekana nadhifu mbele za watu.
Batiki na bazee pia linaweza kushonwa nguo za jinsia zote na kuleta mwonekana aida mwanaume anaweza Shona kinageria mashati Mapana na suluari na mwanamke akavaa gauni fupi au refu au suruali pia mzuri kwa wavaaji hususa ni wanandoa mnapoongozana pamoja.
Mnaweza pia kuchagua nguo za rangi zinazofanana hata kama zitakuwa katika mitindo tofauti bado mtapendeza.
Hapa mwanamke anaweza kuvalia nguo yake yoyote ili Kwenda sambamba na mwenzi wake basi ataangalia moja ya rangi zilizopo katika gauni hilo na yeye akavaa shati na wote wakaonekana nadhifu na watanashatina wakapendana.
Wakati mwingine si lazima kuvaa nguo zinazofanana bali pia mwanaume anaweza kutumia tai yenye rangi zinazofanana nguo ya mwenzi wako, unaweza kuvaa tai ndefu au fupi ili mradi iwe na rangi ambazo zipo katika nguo ya mwezi wake.
Kwa kufanya hivyo muda wote wew na mpenzi wako mtaonekana mnapendeza na kuvutia machoni kwa watu.