JK uso kwa uso na wanariadha vinara

RAIS Mstaafu  Jakaya Kikwete amekutana na Wanariadha Gabriel Geay na Wence Tarimo walioshiriki katika Mashindano ya Riadha yaliyofanyika Boston, Marekani  Aprili  17, 2023.

Gabriel Geay aliibuka mshindi wa pili katika mashindano hayo.

Mheshimiwa Rais Mstaafu amempongeza Gabriel Geay kwa ushindi mkubwa na kwa kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.

Advertisement

Pamoja na wanariadha hao, walikuwepo pia wahamasishaji mbalimbali akiwemo “Bongo Zozo”.

Aidha, amewapongeza pia kwa kuhamasisha ushindi huu na kufanikisha kuinua bendera ya Tanzania juu.

Rais Kikwete yuko Boston, Marekani ambapo anashiriki katika kutoa mafunzo kwa Mawaziri wa Fedha kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea kupitia Mpango wa Uongozi wa Harvard “Harvard Ministerial Leadership Program”.

Katika mafunzo hayo, Saada Mkuya, Waziri wa Fedha wa Zanzibar ameshiriki

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *