JK: Wataanza kufa wao niwazike

RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amebainisha kuwa kitendo cha kuanika ukweli kuhusu maendeleo makubwa yaliyofanywa na Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ndiyo yamewafanya baadhi ya watu kusema maneno ya ajabu, ikiwemo kudai kuwa yeye amekufa au anapaswa kupumzika.

Hata hivyo, Kikwete amebainisha hadharani kwamba hajafa, haugui popote na wala hajaamka na kichomi na kwamba wale wote wanaomuombea mabaya watakufa wao yeye ndio atakayeenda kuwazika.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Bagamoyo, mkoani Pwani, Kikwete alisema baadhi ya watu wanadhani kwa sababu anazungumza kuhusu mafanikio makubwa ya CCM, basi labda amechoka kisiasa au amekufa jambo ambalo alisema si kweli hata kidogo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button