JKT Queens kambini kujiwinda na Ligi ya Mabingwa Afrika
JKT Queens imeingia kambini kujiandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake inayotarajiwa kuanza mapema Novemba nchini Algeria.
Timu hiyo ilipata nafasi ya kushiriki michuano hiyo baada ya kutwaa ubingwa wa Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Akizungumza na gazeti la HabariLEO, Msemaji wa JKT Tanzania na JKT Queens, Masau Bwire amesema timu hiyo inaanza kambi ya ndani leo hadi Oktoba 12 na baada ya hapo itakwenda kuweka kambi nje ya nchi.
“Kesho (leo) ni mwanzo wa maandalizi yetu rasmi. Kambi ya ndani itaendelea hadi Oktoba 12 na baada ya hapo tutasafiri hadi nchi yenye hali sawa na ya Algeria, ambapo mashindano yatafanyika,” amesema Masau.
Amesisitiza timu hiyo inajiandaa kikamilifu kuwania ubingwa huo, lengo likiwa ni kuleta heshima kwa Tanzania na Ukanda wa Cecafa.
“Lengo letu ni kushinda na kufikia hilo kunahitaji maandalizi ya kina. Tumejitoa kuhakikisha timu yetu inashindana kwa kiwango cha juu,” amesema.
Masau pia ametoa wito kwa Watanzania kuungana na JKT Queens katika harakati za kutafuta ubingwa wa Afrika.




Every month start earning more than $12,000 by doing very simple Online job from home.i m doing this job in my part time i have earned and received $12429 last month .I am now a good Online earner and earns enough cash for my needs. Every person can get this Online
job pop over here this site… https://Www.Salary7.Zone