KLABU ya Simba leo inaikaribisha JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania kwenye uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram JKT Tanzania imeandika; “Hatimaye siku ya kuwachapa kichapo cha kizalendo Simba imefika. Tunaomba mamlaka na taasisi zote zisiingilie huu ugomvi wetu. TUNAWEZANA💪 SISI HAWA TULIKUWA TUWATAKA SANA LEO TUMEWAPATA.”