KENYA : MAHAKAMA Kuu nchini Kenya imepinga maamuzi ya wabunge kumuondoa madarakani Naibu Rais Rigathi Gachagua na imeomba mchakato huo upelekwe kwa mwanasheria mkuu kwa ajili ya kutoa muongozo wa kusikiliza kesi hiyo.
Jaji Lawrence Mugambi amesema kwa kuzingatia maslahi ya umma kwenye kesi hiyo kunahitajika kuundwa jopo la majaji ili watazame hoja ya kumuondoa madarakani Gachagua.
Maamuzi ya Mahakama Kuu yametolewa baada ya Jumanne wiki hii bunge kupiga kura kuunga mkono kuondolewa madarakani kwa naibu huyo wa rais, kwa tuhuma za kuhusika na ufisadi na uchochezi wa chuki za ukabila.
Baraza la Seneti la Kenya linatarajiwa wiki ijayo kujadili tuhuma hizo na kupiga kura ya kuunga mkono kumuondoa au kumbakisha madarakani Naibu Rais Gachagua.
SOMA : Bunge la Kenya kumjadili Rigathi