Kampuni ya Bima ya Jubilee imezindua huduma ya bima kwa makampuni ya utalii nchini
Tanzania.
Hatua hiyo itasaidia makampuni ya waongoza utalii nchini, kupata ahueni, pindi majanga kama vile ajali na uharibifu wa vyombo vya moto utakapotokea.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo jijini Arusha juzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Jubilee Insurance Tanzania, Dipankar Acharya amebainisha umuhimu wa ‘bima ya dhima’(liability insurance) katika sekta hiyo yenye thamani ya dola bilioni 2 kwa mwaka.
Afisa Mtendaji Mkuu huyo, amedokeza umuhimu wa huduma hiyo, hususan kwa makampuni yenye kuhudumia wageni kutoka nchi za nje.
“Kampuni yoyote ya utalii inaweza ikijikuta kwenye wakati mgumu sana kibiashara na kiuchumi iwapo hawatakuwa wamejikatia bia ya aina hii,” alieleza.
Kulingana na bwana Acharya, huduma ya ‘bima ya dhima’ inamlinda mmiliki wa kampuni ya utalii dhidi ya kesi na fidia kubwa zitakazojitokeza pindi wateja wao watakapokuwa wamehusika katika ajali au tatizo lolote ndani ya magari yao.
“Huduma hii italeta ahueni ya kweli kwa mmiliki na hatimaye kumpa mmiliki utulivu wa akili
katika biashara yake,” aliongeza.
Aidha, bwana Acharya amewarai waongoza utalii wote na wadau wote kwenye sekta hiyo kuchangamkia fursa hiyo adhimu, hususani katika kipindi ambacho sekta hiyo inarudi kwa kasi mara baada ya janga la UVIKO 19.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (Tato), Sirili kko ameipongeza kampuni ya Jubilee Insurance kwa kuja na huduma hiyo rafiki, hukuakiwahimiza wajiunge nayo mara moja.