Juhudi kurejesha amani Myanmar hazitoshi

LAOS : VIONGOZI wa mataifa 10 wanachama wa Jumuiya ya Kusini Mashariki Asia waliokutana katika kilele cha mkutano wa Laos nchini wamekosoa juhudi za utekelezaji wa mpango wa kurejesha amani Myanmar ambapo wamesema hazitoshi.

Katika mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewaambia viongozi hao kuwa Marekani ina wasiwasi mkubwa  kuhusu kuongezeka kwa shughuli za hatari zisizokubalika katika eneo la Bahari ya Kusini mwa China.

Blinken amewaahidi viongozi hao Marekani itaendelea kuunga mkono uhuru wa shughuli katika eneo hilo muhimu ambalo ni njia ya bahari ya shughuli za kibiashara.

Advertisement

Naye Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel, amesema China inapaswa kuchukua hatua kutatua mvutano kuhusu suala la ushuru na Umoja wa Ulaya.

Michel ameonya kwamba mvutano huo unahatarisha na kusababisha vita  za kibiashara.