Jukwaa ukuzaji mboga, matunda lazinduliwa

JUKWAA maalum la kikanda la kukuza sekta ya mboga na matunda (horticulture)katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika(COMESA) limezinduliwa rasmi kwa lengo la kuhakikisha mazao ya viazi mviringo,vitunguu na parachichi yanapata soko zaidi Afrika na nje ya bara hilo.

Ufunguzi wa jukwaa hilo umefanywa na Mkurugenzi wa Taasisi Kilele ya Kilimo cha Mama, Mboga, Matunda na Viungo (TAHA) chini ya Mkurugenzi, Dk, Jacqueline Mkindi na Mtendaji Mkuu wa Shirika la COMESA /ACTESA, Dk John Mukuka jijini Arusha na kushuhudiwa na wakulima kutoka mikoa mbalimbali.

Dk Mkindi amesema uanzishwaji wa jukwaa hilo utawezesha wadà u wa tansia ya ‘horticulture’ kikanda kuandaa mpango wa pamoja wa kutatua changamoto za kisekta ikiwemo uwepo wa ushirika wa kibiashara na nchi za Umoja wa Ulaya.
SOMA: Mbogamboga, matunda chanzo cha kipindupindu

Amesema utiaji saini wa mkataba wa jukwaa hilo hilo unatoa fursa ya kupeleka mazao ya parachichi,viazi mzingiro na zaobla parachichi kukua zaidi ikiwemo wakulima kunufaika na kilimo kutokana na mazao wayanyozalisha.
SOMA: serikali yafanya uwekezaji mkubwa mazao ya mboga mboga



