Jumuiya ya Wazazi injini ya chama,

Zawadi Kombe la Wazazi zaanikwa

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Khadija Ally amesema jumuiya hiyo ni kapu linalobeba vijana hadi mwisho, na kwamba ndio injini ya Chama Cha Mapinduzi.

Ameyasema hayo leo Mei 5, 2023 jijini Dar es Salaam kwenye hafla fupi ya kukabidhi  kanuni za Mashindano ya Wazazi Super Cup ambazo zimeanzia ngazi ya kata

Lengo la mashindano hayo ni kuhamasisha malezi bora na maadili  kwa watoto, kuibua vipaji, kuongeza ajira na kuimarisha Jumuiya ya Wazazi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 2020-2025.

Khadija amesema, jumuiya hiyo ni  injini ya gari ya Chama na kwamba bila injini haiwezi kwenda, na injini hiyo sio kukuu kwamba ukitoka Karimjee mpaka Lumumba imechemka unaongeza maji.

Mimi na kamati yangu ya utekelezaji wa mkoa tunakuja kivingine, nina hakika tunakwenda kivingine kuipa thamani jumuiya ya wazazi, ijulikane, iheshimike na tufanye kazi kwa mujibu wa kanuni za chama.”Amesema na kuongeza

“Wazazi super cup haikuwepo siku za nyuma, lengo la kuwa na Kombe la wazazi kuanzia ngazi ya kata, wilaya na mkoa ni kuhakikisha tunaenda kuongeza hamasa ya jumuiya ya wazazi, lakini tunaenda kuongeza uhai wa jumuiya yetu, michezo hii iende kuongeza uhai wa chama katika jumuiya yetu

.

“Naomba katika ngazi za wilaya zote, wanachama walioingizwa kuanzia Junuari mpaka mwezi huu wa tano ni wa ngapi?

“Baada ya hapa nitaomba kufahamu wanachama walioingizwa katika kipindi chote cha michezo tuone kusudio letu kama limetimia, kuongeza hamasa, kuongeza wanachama, kurudisha uhai wa chama na kuzidisha mahusiano kati ya jumuiya na wanachama wake na wananchi tunaoishi nao.”Amesema Khadija

Amesema 2024 kuna uchaguzi wa serikali za mitaa,  hivyo kuanzia sasa wanatakiwa kutengeneza mtaji wa wapiga kura kwa kuongeza idadi ya wanachama.

“Kamati hizi zimeundwa kwa kanuni, kila wilaya ina kamati ya michezo, utamaduni na mazingira, kila kamati itakuwa na jukumu la kuangalia azma inatimizwa.

Mashindano ya kata yameshaanza kutimua vumbi na yatafikia tamati yake Mei 25, mashindano ya wilaya yatafikia tamati Juni 10, 2023 wakati Ligi ya Mkoa itaanza kurindima rasmi Juni 27, 2023.

Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo atapata Sh milioni 5, medali 30 za dhahabu na kombe, wakati mshindi  wa pili atapata sh milion 3,medali 30 za fedha na ngao wakati mshindi wa tatu atapata sh milioni 1.5

 

 

 

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button