Kairuki:Hakuna mradi utakwama Kibamba

Mgombea wa Jimbo la Kibamba liliopo jijini Dar es Salaam kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Angellah Kairuki amesema ataendeleza kwa kasi miradi iliyopo katika jimbo hilo na kusisitiza kuwa hakuna mradi utasimama.

Kairuki ameyasema hayo leo wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu zilizoanza Agosti 28,2025 katika maeneno ya Saranga,Mbezi na Goba.

Amesema ataendelea kuimarisha mshikamano na mshirikiano miongoni mwa wanachama wa chama hicho.

Katika ziara hiyo, Kairuki amebainisha kuwa moja ya vipaumbele vyake ni kuhakikisha changamoto za wananchi zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Ametaja changamoto za soko, maeneo ya kuzikia pamoja na barabara kuwa ndizo zinazowakabili wakazi wengi wa Kibamba.

“Nitaendeleza kasi tuliyoanza, hakuna mradi wowote utakaosimama. Nitahakikisha wananchi wa Kibamba wananufaika na maendeleo ya kweli,” amesema Kairuki.

Amesisitiza kuwa dhamira yake kubwa ni kuwalipa wananchi kwa uwajibikaji, kusikiliza sauti zao na kuwapigania ili jimbo la Kibamba liendelee kusonga mbele.

Amebainisha kuwa mshikamano wa wanachama wa CCM katika jimbo hilo ndiyo chachu ya ushindi na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo inayotarajiwa kuinua maisha ya wananchi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button