DAR ES SALAAM: Mrembo kutoka tasnia ya filamu nchini Frida Kajala ameeleza kuwa anamshukuru Mungu kwa kujibu maombi yake alimuomba apate mchumba na amepata.
Akizungumza na habari leo jijini Dar es Salaam, Kajala amesema alimuomba sana Mungu apate mchumba ambaye siyo maarufu na Mwenyezi Mungu amejibu maombi yake hivyo anajihisi mtu mwenye furaha na amani katika maisha yake.
“Kwenye maombi yangu nilimuomba Mungu anijalie mchumba ambaye sio maarufu na mcha Mungu nimempata japo wengi wanatamani kumfahamu mtamfahamu.”amesema Kajala.
Ikumbukwe Msanii huyo kipindi kilichopita alikuwa kwenye mahusiano na Star wa Muziki wa Bongofleva Rajabu Abdukahari ‘Harmonize’ kabla ya wawili hao kuachana na sasa Kajala anaweka wazi kuwa tayari yupo kwenye mahusiano mapya.