Kalemani, Makongo kuchuano ubunge Chato

CHATO: MBUNGE wa Chato, Medard Kalemani anatarajia kukutana na upinzani jimboni hapo kuelekea Uchaguzi Mkuu baada ya mwandishi wa habari nguli, Cosmas Makongo kuonyesha nia ya kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Cosmas Makongo ni mwaandishi wa habari za uchunguzi mstaafu aliwahi kuwa mwandishi wa habari wa Hayati Dk John Pombe Magufuli wakati akiwa Mbunge na Waziri wa Ujenzi.

Makongo ametangaza nia ya Kugombea Ubunge wa Jimbo la Chato Kaskazini akiahidi kumg’oa mbunge  Dk Medard Kalemani kwa madai kwamba anastahili kupumzika baada ya kuwatumikia wananchi katika kipindi cha miaka 10.

Amesema kuwa ameamua kugombea ubunge kwa madai kwamba wakati huu jamii inahitaji nguvu kazi mpya ili kuendeleza utekelezaji wa Ilani ya CCM, ushirikishwaji wa wananchi kwenye mamabo ya msingi, kuwasemea wananchi changamoto,kuwapambania ili wanufaike na fursa za Serikali.

Mwandishi wa habari nguli nchini Tanzania Cosmas Makongo ambaye pia ni mazaliwa na mkazi wa Buzirayombo mkoani Geita, ni miongoni mwa waandishi wa habari mahiri kuwahi kutokea nchini Tanzania ambao wameacha historia kubwa katika habari za uchunguzi.

Miongoni mwa habari ambazo amewahi kuchunguza na kuandika na mwisho wa siku zikaleta athari chanya nchini Tanzania na ukanda wote wa Afrika ya Mashariki ni pamoja na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).

Makongo anajulikana Kwa misimamo yake mikali ya kupingana na unyanyasaji wa aina yoyote ile katika jamii hali ambayo mara kadhaa imemsababisha kujikuta katika wakati mgumu kutoka kwa baadhi ya viongozi hapa nchini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button