DAR ES SALAAM; KAMATI ya Kupokea Maoni, taarifa na Kushughulikia Malalamiko ya Uhalifu katika Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi ( HEET), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, imezinduliwa leo.
Naibu Mratibu wa HEET, chuoni hapo Dk Liberato Haule, amesema utekelezaji wa mradi huo, unazingatia ushirikishaji wa jamii unayoizunguka.
Naye Mkurugenzi wa taasisi ya kijinsia chuoni hapo, Dk Lulu Mahali amesema kamati hiyo ina kazi ya kupokea malalamiko yanayohusuana na mradi ikiwa ni pamoja na malalamiko ya jamii iliyozunguka maeneo ya mradi huo.
” Tuna masuala ya unyanyasaji wa kijinsia katika eneo tulilojikita nalo, tunakazana kulizuia, ni eneo la unyanyasaji wa kingono.
“Katika masuala ya jinsia tutakuwa tunapokea taarifa kupitia wadau walioandaliwa wanaofundishwa jinsi ya kupokea maoni, kuyahifadhi na kufikisha taarifa,” amesema.
Ameeleza kuwa malalamiko kama hayo yasipofuatiliwa yanaweza kusimamisha mradi mzima.
Mtaalamu wa Masuala ya Usalama wa Mradi, Dk Edmund Mabuye amesema kamati hiyo iliyozinduliwa inapewa mafunzo maalum ili kuiwezesha ianze utekelezaji rasmi.